Popular posts from this blog
Maisha ya Mtakatifu Filomena wa Roma, FEBRUARI 17, 2019
Filomena wa Roma ( 10 Januari 291 - 10 Agosti 304 ) alikuwa bikira wa ukoo tawala wa Corfu ( Ugiriki ) ambaye alianza kuheshimika kama mtakatifu mfiadini baada ya masalia kupatikana mnamo Mei 1802 katika Mahandaki ya Priscilla , Roma , Italia . Paliandikwa Pax Tecum Filumena (yaani "Amani kwako, Filomena"). Kabla ya hapo hakujulikana, lakini baadaye heshima ya Wakatoliki na Waorthodoksi wengi kwake imestawi sana hadi leo sehemu nyingi za dunia ikisaidiwa na njozi na miujiza iliyotokea kwa kuomba sala zake. Kati ya miaka 1837 na 1961 Kanisa Katoliki liliruhusu heshima hiyo katika liturujia pia. [1] Lakini wasiwasi wa wanahistoria umefanya jina lake liondolewe katika kalenda zote za watakatifu.
TAFAKARI, FEB 10: VILIVYO VIDHAIFU KUPEWA THAMANI YA KUMTANGAZA MUNGU
“MBEGU ZA UZIMA” Tafakari ya kila Jumapili Februari 10, 2019 DOMINIKA YA 5 YA MWAKA WA KANISA VILIVYO VIDHAIFU KUPEWA THAMANI YA KUMTANGAZA MUNGU Jumapili iliyopita tulisikia kuhusu wito wa Yeremia, na leo tuna habari tena ya wito wa Isaya na Petro. Mmoja anaweza kujiuliza kwanini Mungu anachangua watu kama hawa? Mungu anafikiria nini? Lakini ukweli ni kwamba hili sio jambo geni kwa Mungu. Abrahamu alichaguliwa na Mungu akiwa mzee ili awaweze kuwa Baba wa taifa la Israeli, Mungu alimchagua Musa ambaye alikuwa hawezi kuongea vizuri, kigugumizi ili kukabiliana na Farao na kuongoza wana wa Israeli, Kijana mdogo tena mchungaji, Daudi alichaguliwa na Mungu kuwa Mfalme wa Israeli. Na pia Sauli ambaye alikuwa mtesi wa Kanisa anachaguliwa na Yesu kuwa chombo chake kiteule cha kuhubiria Injili yake. Hii yadhihirisha kwamba Mungu anafanya kadiri ya mapenzi yake. Vyombo anavyo vichagua Mungu ni kutoka katika ulimwengu wetu, hata kama sisi tunaviona ni dhaifu. Tunaweza tukak...
Comments
Post a Comment