Maisha ya Mtakatifu Filomena wa Roma, FEBRUARI 17, 2019


Filomena wa Roma ( 10 Januari 291 - 10 Agosti 304 ) alikuwa bikira wa ukoo tawala wa Corfu ( Ugiriki ) ambaye alianza kuheshimika kama mtakatifu mfiadini baada ya masalia kupatikana mnamo Mei 1802 katika Mahandaki ya Priscilla , Roma , Italia . Paliandikwa Pax Tecum Filumena (yaani "Amani kwako, Filomena"). Kabla ya hapo hakujulikana, lakini baadaye heshima ya Wakatoliki na Waorthodoksi wengi kwake imestawi sana hadi leo sehemu nyingi za dunia ikisaidiwa na njozi na miujiza iliyotokea kwa kuomba sala zake. Kati ya miaka 1837 na 1961 Kanisa Katoliki liliruhusu heshima hiyo katika liturujia pia. [1] Lakini wasiwasi wa wanahistoria umefanya jina lake liondolewe katika kalenda zote za watakatifu. 

Comments

Popular posts from this blog

TAFAKARI, FEB 10: VILIVYO VIDHAIFU KUPEWA THAMANI YA KUMTANGAZA MUNGU